
Date: May 27, 2025
Location: Mara Region
Original Report (Swahili):
Aliumwa na mbwa asiyejulikana anayedhaniwa kuwa na kichaa cha mbwa tarehe 28 Februari 2025, majira ya saa 1 asubuhi wakati akielekea shule. Aliumwa mguuni na alipata jeraha dogo. Mama yake alimsafisha jeraha kwa mafuta ya taa kama huduma ya kwanza, kisha wakampeleka kwenye Zahanati ya Iseresere ambako alipatiwa sindano ya pepopunda (TT). Kwa kuwa jeraha lilionekana dogo na hali ya mtoto ilikuwa nzuri, mama yake hakudhani kuwa ni muhimu kupata chanjo ya PEP. Tarehe 26 Mei 2025, Night alianza kuonesha dalili za kichaa cha mbwa kama kuweweseka, kuogopa maji (hydrophobia), kutokwa na mate mengi, na maumivu ya kichwa. Alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Iramba, lakini kwa bahati alifariki kwani dalili zilishakuwa zimeanza. Bint alifariki dunia tarehe 27 Mei saa 11 alfajiri.
Translation:
He was bitten by an unknown dog suspected of having rabies on February 28, 2025, at around 1am while on his way to school. He was bitten on the leg and sustained a minor injury. His mother treated the wound with kerosene as first aid, then took him to Iseresere Dispensary where he was given a tetanus (TT) injection. Since the wound appeared minor and the child was in good condition, his mother did not think it was necessary to get the PEP vaccine. On May 26, 2025, Night started showing symptoms of rabies such as delirium, fear of water (hydrophobia), excessive salivation, and headache. He was rushed to Iramba Health Centre, but unfortunately, he died as the symptoms had already started. The child died on May 27 at 11am.
* This tragic case illustrates the fatal misconception between tetanus vaccination and rabies PEP – minor wounds from suspected rabid animals require immediate PEP regardless of wound size, as rabies is 100% fatal once symptoms appear.